Mpango Maalum kwa Watanzania Waishio Nje
UTANGULIZI
Limekua ni jambo la kawaida na lililozoeleka kwa Mtanzania aishiye nje ya Tanzania kununua mali (properties) kupitia ndugu,jamaa au marafiki waioko Tanzania na kuishia ama kudhulumiwa au kukuta bidhaa dhaifu isiyolingana na matarajio yake.
Mathalani,ndugu,jamaa au rafiki aliyeaminiwa hudanganya kuwa amenunua kiwanja kumbe si kweli au kama ni ujenzi huishia kupiga picha nyumba za watu na kumtumia nguguye wa nje ya nchi huku akiendelea kufaidi fedha anazotumiwa kwa maisha ya anasa bila kufikiria kwamba nduguye huyo anataabika ughaibuni kutafutaa hela ili kuandaa maisha yake ya baadaye.Ndugu huyo inapofikia kipindi cha kurudi nchini hupigwa na butwaa pale anapogundua kuwa alichezewa mchezo mchafu na mtu aliyemuamini.
UFUMBUZI WA TATIZO
Kutokana na tatizo hilo hapo juu,Makazi Investment Ltd imekuja na mpango madhubuti na salama kwa ajili ya watu waishio nje ya Tanzania ili wasiweze ama kudhulumiwa au kununuliwa/kuuziwa bidhaa dhaifu.
Mpango huo utazihusisha pande tatu:
1.Mnunuzi aishiye nje
2.Ndugu/Jamaa/Rafiki anayeaminiwa
3.Kampuni ya Makazi (Makazi Investment Ltd)
Jinsi tunavyofanya:
-
Mnunuzi aishie nje akishafanya maamuzi ya kununua kiwanja au nyumba au kufanya ujenzi atawasiliana nasi.
-
Atamtambulisha kwetu msimamizi wake(Ndugu/jamaa au rafiki) na kututambulisha kwa huyo mhusika kwamba anataka kununua toka kwetu.
-
Tutaunda kundi la whatsapp kwa ajili ya mpangokazi uliyo mbele yetu.
-
Jukumu la kampuni ni kutoa huduma husika kama ambavyo mnunuzi anahitaji na kumdhibiti msimamizi kuhakikisha kuwa kile anachopewa ndicho kinachohitajika na kwamba kile anachonunua ni cha thamani na ubora uliokubaliwa na pia kuhakikisha kuwa nyaraka za mali husika ni za mlengwa na si vinginevyo.
-
Kazi ya msimamizi ni kuhakikisha na kuidhibiti kampuni ili itoe huduma iliyokubaliwa na kwa ubora stahiki.
-
Kila jambo linalofanyika taarifa yake itatolewa kwenye kundi la whatsapp ili pande zote tatu kufahamu na kuhakiki.Kama ni picha za kiwanja husika,nyumba husika au nyumba iliyoko kwenye ujenzi vyote vitapitia katika kundi hili ili kila pande ithibitishe kuwa ni kweli.
-
Mawasiliano yote yatakwenda kwa mfumo huu hadi siku Mmiliki atakapokuja nchini na kukabidhiwa mali yake ikiwa salama na kwa ubora uliokusudiwa.
Ni matumaini na matarajio yetu kuwa kuanzia sasa mtu kudhulumiwa au kudanganywa itakuwa ni maamuzi yake kwa uzembe wake lakini si kwa bahati mbaya.