top of page
LIPIA KIWANJA KIDOGOKIDOGO KUANZIA TSH 7,000/- KWA WIKI

Mpendwa mteja wetu wa thamani!

Salaam!

Kwanza nikushukuru sana kwa kuwa mteja wetu.Ni jambo la furaha na fahari kuona kwamba wewe ni mmoja wa watu waliotufanya tufanikishe biashara yetu.

Kwa sababu ya thamani uliyonayo kwetu;na kwa kutambua kuwa ardhi ni uwekezaji ambao tamani yake inaongezeka kila siku;tumekuja na mpango mahsusi kwa ajili yako ili kukufanya uwekeze kwa wepesi kabiasa katika viwanja vilivyoko kwenye miji yetu ya mbali (satellite towns) katka maeneo ambayo tayari tunajua kuwa katika mipango ya baadaye patakua na maendeleo mazuri sana.

Mfano mradi wa kwanza kwa ajili ya wateja wetu endelevu uko Bagamyo Kiwangwa jirani na Msata;kilometa mbili kasoro toka Bagamoyo Road.

Eneo hili liko jirani na eneo lililotenga kwa ajili ya Chuo Kikuu cha IFM kwa siku za baadaye na pia limepakana na viwanja vya watu wa SACCOSS ya Posta na Simu (Waliuziana mamia kwa maelfu ya viwanja)

Hili ni mojawapo tu ya maeneo hayo lakini tutakua na maeneo mbali mbali mfano Chalinze,Lugoba,Pongwe,Mlandizi na kwingineko ambayo yote yatakua na viwanja kwa ajili hiyo.

HABARI NJEMA:

Habari njema ni kwamba utakua na uwezo wa kuwekeza kwa kulipia kiwanja chako kwa kiwango cha chini kabisa hadi Tsh 7,000/- (Elfu Saba tu ) kwa wiki kwa kiwanja cha ujazo wa sqm 400.Malipo hayo kwa wiki yataongezeka kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa kiwanja Zaidi ya sqm 400.Kwa mfano kama sqm 400 utalipia 7,000 kwa wiki basi kiwanja cha sqm 600 utalipia Tsh 10,500 kwa wiki;cha sqm 800 utalipia Tsh 14,000 kwa wiki nk.

Unaruhusiwa kununua idadi yoyote ya viwanja kwa kadiri upendavyo.

KWA NINI UNUNUE KIWANJA CHA BEI NAFUU ILHALI UNA MAISHA MAZURI NA JUMBA LA KIFAHARI?

Najua ni wengi wenu wanajiuliza swali hilo.Kwamba masuala ya kununua viwanja tayari ulishaachana nayo.Si kweli.

Kuna faida nyingi;

 

1.UWEKEZAJI – Kwa sasa utakinunua kiwanja kwa bei rahisi lkn baadaye hutaamini utakapokuta bei yake imepanda zaid ya mara kumi ya sasa.Mfano umechukua viwanja 10 unavilipia 70,000 kwa wiki….baada ya miaka labda mitano hadi kumi ijayo unaweza ukajikuta unamiliki vianja vyenye thamani ya Zaidi ya milioni 100 ambavyo ulivipata kwa urahisi kabisa.

 

2.UWEZESHAJI – Umewahi kuwafikiria wafanyakazi wako ambao wanafanya baadhi ya kazi zako na hawana matumaini kabisa ya kumiliki kiwanja katika maisha yao?Fikiria mshahara wa wafanyakazi wako kama Housegirl,Houseboy,Gateman nk ilivyo midogo.Haw hawana matumaini kabisa ya kumiliki chochote cha thamani hasa kiwanja;lkn kupitia mpango huu unaweza kuwawezesha ama kama zawadi au kwa makato madogomadogo

 

3.ZAWADI – Kule ulikotoka una ndugu na jamaa wenye hali duni ambao wala hawajawahi kufikiri kumiliki kiwanja maeneo ya karibu na jiji la Dar es Salaam…kuna watu Fulani unawafahamu wanapitia

katika changamoto kubwa ya kimaisha;huu ndi wakati muafaka wa kuvuna BARAKA zako kwa kuwanunulia viwanja.

 

4.MABADILIKO YA KIUCHUMI – Wapo watu waliingia kwenye mgogoro wa kiuchumi kiasi kwamba nyumba zao ziauzwa au wakalazimika kuziuza,anaanza kujiuliza ataanzaje maisha…lakini iwapo umenunua kiwanja kwa njia nafuu na kukiacha likitokea jambo kama hilo huwezi kuwa mashakani kamwe.

Ziko faida nyingi sana za mpango kwako kupiti mpango huu wa uwezeshaji wa umiliki wa viwanja kwa njia nafuu na rahisi.

UTARATIBU:

Utachagua kiwanja kwenye ramani kisha utajaza fomu ambayo inalipiwa Tsh 10,000/- (Elfu Kumi tu) baada ya hapo utapewa maelekezo ya jinsi ya kulipia,utakilipia kiwanja kidogokidogo kila wiki(lakini unaruhusiwa kulipa Zaidi ya kiwango cho hata ukitaka kulipa cash kutakua na punguzo) hadi utakapofikisha NUSU YA THAMANI YA KIWANJA ndipo utakwenda kukabidhiwa kiwanja chako,utaruhusiwa kuendelea kukifanyia maendeleo ikiwemo ujenzi na kadhalika wakati ukiendelea kumalizia nusu iliyobakia.

Bei ya kiwanja kwa sqm ni Tsh 3,000 (elfu tatu) na tunatarajia iwapo mteja atalipia kwa kiwanja elekezi basi malipo yake yatakamilika ndani ya miaka mitatu.

 

Summary:

Mfumo wa ununuzi wa viwanja vya Tsh 7,000 kwa wiki
1.Chagua kiwanja na kujaza fomu (Unaweza kufika  ofisini au ukafanyia mtandaoni)
2.Saini mkataba wa kisheria ofisini (Utathibitishwa na Wakili/Mwanasheria)
3.Anza kulipia Tsh 7,000 kila wiki kupitia bank (Utapewa akaunti ya kampuni)
4.Miezi 6 ikitimia utapelekwa site kuona kiwanja 
5.Endelea kulipia mpaka deni liishe
6.Malipo ni ndani ya miaka mitatu Bei kwa sqm ni Tsh 3,000 tu)

7.Ukitaka kulipa cash bei ni Tsh 800,000 kwa kiwanja cha sqm 400 (Tsh 2,000 kwa sqm)

KUMBUKA:

Hata Manzese,Sinza,Ubungo,Kimara,Boko,Bunju na kwingineko zamani palikua panaonekana ni porini.Kutokana na ujenzi wa Bndari ya Bagamoyo tunatarajia maendeleo makubwa zaidi kutoka Bagamoyo kuelekea Msata kwani upande huo uko juu ya kina cha maji (Water Bed) tofauti na upande uliopo kati ya Bagamoyo na Dar es Salaam ambao hautaweza kuhimili majengo makubwa na mazito na pia umetengwa kwa asilimia kubwa kwa ajili ya viwanda.Makazi ya watu wa hali ya kawaida na makazi ya kifahari yote yanategemewa kuwa upande huo wa kuelekea Msata.Pia Vyuo Vikuu vingi vya Jijini Dar es Salaam vimeandaa maeneo upande huo kwa ajili ya kujenga majengo yao makubwa na ya kudumu upande huo.

Ukweli halisi ni jinsi upande huo kulivyo na miji inayokua kwa kasi ya ajabu mfano Makurunge,Kidomole,Fukayosi,Mwavi,Kiwangwa,Mwetemo,Masuguru na Msata.

MAELEZO ZAIDI:

Fika ofisini Makazi Investment Ltd ili kupata maelezo zaidi au tupigie 0713565999/0767565999 kwa ajili ya maswali yoyote.

Ofisi zetu zipo Kijitonyama,Jengo la Mwanga (Mwanga Tower),Ghorofa ya 5.

 

bottom of page