top of page

MATANGAZO

MAKAZI INVESTMENT LTD

Makazi Investment Limited, ni kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria ya makapuni ya mwaka 2002, kampuni hii inahusika na kazi za uuzaji na ununuzi wa viwanja, kurekebisha viwanja pamoja na shughuli zote za upimaji wa ardhi.

 

 

Makazi Investment Limited ina ofisi mbili, ambapo ofisi kuu ipo mtaa wa bwawani, kijitonyama karibu na kituo cha mabasi makumbusho na ofisi nyingine ndogo ipo mtaa wa sheli, kiwalani.

 

 

Ndani ya Makazi Investment, lengo kuu daima limekua kuwasaidia watanzania hasa wale wenye kipato cha kawaida kuwa na uwezo wa kumiliki ardhi; na hili limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kupitia mpango wetu ya kukopesha viwanja kwa masharti nafuu kabisa na kumfanya mteja akalipa kidogo kidogo ndani ya kipindi ambacho tutakua tumekubaliana.

 

 

Kumpitia mpango huo wa ukopeshaji wa viwanja katika sehemu mbali mbali za mji wa dar es salaam na maeneo ya pembezoni; Makazi Investment Limited imefanikiwa kurahisisha maisha ya watanzania walio wengi na kuwafanya wawe na uwezo wa kujenga.

bottom of page